Wakrito
nchini na watanzania wametakiwa kuliombea taifa ili liweze kuvuka
salama kipindi hiki kigumu chenye matukio makubwa ya upatikanaji wa
katiba mpya pamoja na uchaguzi mkuu huku viongozi wakitakiwa kutenda
haki kwani amani ni tunda la haki.
Askofu wa kanisa la AICT dayosisi ya Pwani Charles Salalah ametoa
wito huo wakati wa ibada ya ijumaa kuu ambayo kitaifa imefanyika katika
kanisa la AICT magomeni jijini Dar es Salaam ambapo amesema maeneo yote
duniani ambayo yamekumbwa na machafuko chanzo kikubwa ni ukosefu wa haki
hivyo ni wajibu wa kila kiongozi mwenye dhamana kutenda haki.
Ibada hiyo imehudhuriwa na wachungaji kutoka madhehebu mbalimbali
ambayo pia imetumika kuliombea taifa pamoja na viongozi mbalimbali
akiwemo rais Jakaya Kikwete ili mungu amjalie afya njema aweze
kuliongoza taifa vyema sala iliyoongozwa na mchungaji Daniel Ntebi.
Katika kanisa la KKKT Azania Front ibada ya pasaka imefanyika na
kupambwa na maigizo yaliyokuwa yanaonyesha mapito aliyopitia bwana yesu
kristo hadi alipokufa msalabani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kifo
chake huku waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa ambaye amehudhuria
ibada hiyo akizungumzia siku hii.