Raheem
 Sterling ataanzishwa katika mechi dhidi ya Arsenal siku ya jumamosi 
licha ya onyo kutoka kwa Brendan Rodgers kwamba kilabu hiyo ya Anfield 
inakabiliwa na changamoto ya kuwazuia wachezaji wake wazuri kuondoka.
Mkufunzi
 huyo wa Liverpool amethibitisha kuwa Raheem atachukua mahala pake dhidi
 ya Arsenal licha mchezaji huyo wa miaka 20 kukiri kwamba anahusishwa na
 kilabu ya Arsenal.Sterling ambaye anarejea katika mchuano muhimu wa Liverpool ambao huenda ukaaamua iwapo kilabu hiyo itacheza katika kombe la vilabu bingwa Ulaya amekataa mkataba wa pauni 100,000 kwa wiki.
Hatahivyo Rodgers atamuanzisha mchezaji huyo dhidi ya kilabu hiyo inayopanga kumnunua mwishoni mwa msimu huu.
