Katikati ya Jiji Dar es Salaam ni mfano mzuri kwamba japo watu wengi
wanatumia magari na pikipiki au bajaji, lakini wapo pia ambao utakutana
nao wakitumia usafiri wa baiskeli.. sasa mtu wangu hiyo sio BONGO
pekeake ambapo watu wanaingia na baiskeli katikati ya miji na kuendelea
na dili zao kama kawaida.
Hapa nimekutana na hii record ambayo imetoka mwezi huu MARCH 2015,
unajua miji au majiji ambayo yametajwa duniani kwamba ndio salama zaidi
kwa kuendesha baiskeli.
No.1: Amsterdan, Netherlands. Miundombinu za mji huu zinafanya zaidi ya 38% ya watu wanaoingia town wanaingia kwa usafiri wa baiskeli.
No.2: Copenhagen, Denmark.
Wao pia wana barabara nzuri kabisa pembeni ya barabara za magari ambazo
wanatumia waenda kwa miguu na waendesha baiskeli. 36% ya watu wanaoenda
shuleni, maofisini kwingineko wanatumia zaidi baiskeli.
No.3: Utrecht, Netherlands.
Record inaonesha 33% ya watu wanatumia baiskeli kwenye safari zao za
kila siku, wakati 19% tu ya watu wamatumia usafiri wa magari.
No.4: Seville, Hispania. Nao pia wamekuwa wakitegemea sana usafiri wa baiskeli kutokana na kuwepo barabara ambazo zinawapa uhuru kuenjoy usafiri huo.
No.5: Bordeaux, Ufaransa, Barabara
ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya waendesha baiskeli ni kama km 200
katikati ya Mji. Hii imefanya kuwepo na ongezeko la watu wanaopendelea
kutumia usafiri huo. Ufaransa ni moja ya nchi walio serious kabisa Ulaya
kuhakikisha mazingira mazuri ya usafiri wa Baiskeli.
No.6: Malmo, Sweden.
Malmo ni mji wa tatu kwa ukubwa Sweden, wao mpaka zile barabara za
baiskeli wamezipa majina, kama ilivyo kawaida kwa barabara kubwa magari.
Waliamua hivyo iwe rahisi kwa mtu kuupata mtaa kwa kutumia GPS.
No.7: Montreal, Canada.
Barabara za mji wao ziko poa kabisa, japo ni mji mkubwa na uko busy
lakini mazingira yanaruhusu hata kwa mwendeshaji wa baiskeli kuwa salama
kabisa.
No.8: Tokyo, Japan.
Huu ni mmoja ya miji mikubwa duniani, wao wameweka utaratibu wa njia za
baiskeli kutumiwa na wapita njia pia. Japo mfumo wa usafiri wa gari na
treni za abiria uko vizuri kuuzunguka mji lakini watu wengi hupendelea
pia baiskeli.
No.9: Rio de Janeiro, Brazil.
Kwenye mafanikio waliyonayo wamefikia hatua ya kuweka mfumo wa baiskeli
za kuazimisha, yani mtu anaichukua akimaliza mizunguko yake anairudisha
na halipii gharama yoyote.