BAADHI YA VIJANA WA JIJI LA MWANZA WAKIWA KATIKA UFUNGUZI WA KAMPUNI YA BEGA KWA BEGA MICROFINANCE....>>>>>
Vijana nchini wameshauriwa kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika maeneo yao ili waweze kumiliki rasilimali zilizopo na kumiliki uchumi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa jijini mwanza na afisa maendeleo ya jamii damas mkama wakati akifungua huduma ya utoaji wa mikopo kwa kampuni ya
bega kwa bega microfinance
Akizungumza kwa niaba ya fisa maendeleo wa jiji afisa vijana juma samweli amesema hatua hiyo itawasaidia kujiimalisha kiuchumi kwa maisha yao ya sasa na baadaye.
Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya bega kwa bega microfinance albert girenga amesema kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuwawezesha vijana wenye ujuzi na wasio na ujuzi kuweza kujiajili.
Amesema kuwa lengo hilo litafikiwa kupitia mikopo itakayotolewa na kampuni hiyo kupitia mikopo ya anzisha na imarisha.
VIJANA WAKIENDELE KUJIFUNZA.
Awali mkurugenzi wa ubunifu na ugunduzi kutoka kampuni ya godtec aloyce midelo amesema kuwa nia ya godtec ni kuinua kipato cha mwananchi wa hali ya chini kupitia huduma ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (poso)
Musa magari ni muuzaji wa bidhaa za mitumba amesema kuwa ukopaji wa vikundi umechangia kuwarudisha nyuma baadhi ya wafanyabishara kutoka na baadhi ya watu kutokuwa waaminifu.