BET Network imemtangaza kumwajili Mtanzania Kay Madati kama makamu mkuu
wa rais (Executive Vice President) pia Chief Digital Officer wa burudani
BET lililoko chini ya kampuni ya Viacom Inc..>>>>
Kufuatia uteuzi huo, Madati atakuwa na kazi ya kuziongoza timu zote za
BET kwenye mitandao ya kijamii na mitandao mingine inayounganishwa na
BET.com (BET Networks), pia katika uzalishaji wa vipindi na uendeshaji
wa teknolojia na bidhaa.
“We are thrilled to welcome Kay to the team, and look forward to his
expertise and strategic leadership in the fast-paced world of digital
and social media, as consumers continue to turn to BET to discover what
is hot and what is next,” alisema Mwenyekiti mtendaji wa BET, Debra L.
Lee.
Madati atakuwa chini ya mwenyekiti huyo mtendaji wa BET.