Mchezaji
wa zamani wa timu ya taifa ya England na Manchester Utd, Phil Neville
amemtetea Yaya Toure wa Manchester City kwa kusema kuwa mwanandinga huyo
si kikwazo kwa klabu hiyo ya jiji la Manchester kutokana na matokeo
mabaya walioyapata katika mchezo wao wa Jumapili. Nevill akizungumza
katika mjadala ulifanyika katika studio za BBC, amesema kuwa kocha
Manuel Pellegrini ndiye aliyekatika wakati mgumu kutokana na kichapo
hicho walichokipata kutoka kwa mahasimu wao wa jiji Manchester Utd, huku
akiamini kuwa kocha huyo ndiye wa kulaumiwa kutokana na maamuzi yake
yasiozaa matunda aliyoyafanya kuelekea katika mchezo huo.
Manchester
City ilibamizwa bao 4-2 na Manchester Utd huku vijana hao wa Etihad
wakifikisha michezo sita kupoteza kati ya michezo nane.