Ikiwa
siku ya kwanza ya zile tatu za maombolezi zilizotangazwa na rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya imeanza kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha
Garissa,makanisa yote nchini Kenya yatajitolea kuwaombea waathiriwa wa
tukio hilo wakati huu wa sikukuu ya pasaka.
Shambulizi hilo la siku ya Alhamisi liliwaacha takriban watu 150 wakiwa wameuawa.Shirika la msalaba mwekundi nchini Kenya linasema kuwa hadi sasa maiti 54 zimetambuliwa katika chumba kimoja cha kuhifadhi maiti kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa idara za usalama zinahitaji kuongeza jitihada za kupambana na wanamgambo wa Al shabaab.
Chuo cha kutoa mafunzo ya kiislamu kinacheshimiwa zaidi nchini Misri, Al-Azhar kimelaani kile ilichokitaja kuwa shambulizi la kigaidi dhidi ya wanafunzi wasio na hatia.