Madai yameibuka kuwa shirika la usalama wa safari za ndege barani Ulaya
 lilielezea wasi wasi wake kuhusu kasoro kwenye sheria za usafiri wa 
ndege nchini Ujerumani kabla ya kutokea kwa ajali ya ndege ya shirika la
 Germanwings mwezi uliopita.
Shirika hilo liliiambia halmashauri 
ya safari za ndege ya Ujerumani mwezi Novemba kutatua matatizo yakiwemo 
ya uhaba wa wafanyikazi hali iliyotatiza shughuli za ukaguzi wa ndege 
pamoja na wafanyikazi wake.Rubani Andreas Lubitz aliiangusha ndege yake makusudi ambapo abiria wote 150 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia.
Utawala nchini ufaransa unasema kuwa umemaliza shughuli za kutafuta mabaki katika eneo la ajali.
