Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Margaret Chan ametoa wito
siku ya Jumatano kuitaka dunia kuondoa tumbaku katika biashara na
kusisitiza mafanikio ya kuachana na uvutaji katika mataifa mengi.
Akizungumza katika Mkutano wa Ulimwengu dhidi ya Tumbaku au Afya mjini
Abu Dhabi, Chan alikaribisha mapendekelo yaliyotolewa na mataifa kadhaa,
ikiongozwa na Australia, iliyoanzisha kutoa pakeji tupu za sigara.
Alitaka hatua hizo kufanywa na mataifa mengine.
Makampuni ya tumbaku “hutumia mbinu mbalimbali zikiwemo kuvipa fedha
vyombo vya siasa, wanasiasa binafsi kufanya kazi kwa ajili yao…
hawatoacha kufanya kuzorotesha jitihada za serikali kutaka kuokoa watu
wao,” Chan aliwaambia waandishi wa habari.
“Yatakuwa mapambano makali… lakini hatupaswi kukata tama mpaka tuhakikishe biashara ya tumbaku inatokomea,” alisema.
Pamoja na kushuka kwa idadi ya wavutaji katika mataifa mengi, jitihada
zaidi zinapaswa kufanyika kupambana na matumizi ya tumbaku ili kupunguza
matumizi kwa asilimia 30 ifikapo 2025,” walisema washiriki.