Mahakama ya katiba nchini Ujerumani imepitisha uamuzi wake kuhusu mavazi
ya kiislamu ya wanawake katika jimbo la Bremen walimu walipewa ruhusa
ya kuingia darasani wakiwa wamevalia hijabu.
Kulingana na taarifa ya maandishi iliyotolewa na Wizara ya Elimu na
Sayansi katika jimbo la Bremen kuwa hakuna haja ya kupigwa marufuku
maana mavazi hayo hayahusiani na kitisho cha ugaidi.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa walimu kuvalia hijabu haina hatari yoyote
wala hakiwezi kuwa kitisho cha amani kwa shule za Bremen.