Balozi KHAMIS KAGASHEKI
Wakaazi wa Manispaa ya Bukoba Mkoani KAGERA wametakiwa kujitokeza
katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
,pamoja na kuipigia kura katiba inayopendekezwa ikiwa ni sehemu ya
kutekeleza haki yao ya kikatiba .
Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini ,Balozi KHAMIS KAGASHEKI katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kashai manispaa ya Bukoba, ambapo amesema wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mambo mbalimbali ya maendeleo ya nchi.
Balozi KAGASHEKI ameelezea utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi katika manispaa hiyo Ikiwemo kuondoa kero mbalimbali ,kama vile kuongezwa kwa muda wa kulipia usajili wa pikipiki za abiria, pamoja na kurejesha huduma ya umeme katika soko la KASHAI,
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoani KAGERA ALI AME anasema Chama cha Mapinduzi kimefanya mengi licha ya baadhi ya vyama kubeza na kutaka kuilinganisha TANZANIA na baadhi ya mataifa yaliyoendelea.