Mikel Arteta
|
1982: Mikel Arteta azaliwa
Huyu ni
nahodha wa klabu ya Arsenal(England) akiweka rekodi ya kutoichezea timu
ya taifa ya Hispania (La Roja) alizaliwa Donostia, San Sebastian.
Alianza soka lake na FC Barcelona, baadaye akatolewa kwa mkopo PSG.
Amewahi kuichezea Rangers ya Uskochi msimu wa 2002-03 wakitwaa mataji
matatu kwa pamoja. Pia Real Sociedad ambako hakukaa sana. Msimu wa
2004-05 alitolewa kwa mkopo Everton. Mwaka 2011 alisajiliwa na ‘Washika
Bunduki’ wa London na Agosti 2014 aliteuliwa kuwa nahodha wa timu hiyo.
1974: George Foreman amtandika Ken Norton TKO
Bondia wa
zamani nchini Marekani George Foreman ambaye alitwaa medali ya dhahabu
katika Michuano ya Olimpiki ya mwaka 1968 nchini Mexico alimzabua Ken
Norton kwa TKO, kabla ya kupoteza dhidi ya Joe Frazier. Pia alipigwa na
Muhammad Ali katika ‘Rumble in the Jungle’. Kabla hajastaafu alishinda
mapambano 76 na kupoteza 5. Jarida la ‘The Ring’ limemuweka nafasi ya 9
katika orodha ya watupa mawe wa zama zote.
1992: Mike Tyson ahukumiwa miaka 10 jela
Mkali huyu
aliyeweka rekodi ya kutetea taji lake mara 9 likiwemo pambano dhidi ya
Larry Holmes na Frank Bruno, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada
ya kumbaka mwanadada mrembo Desiree Washington. Mwaka 1990 alipoteza
taji lake dhidi ya James ‘Buster’ Douglas kwa KO katika raundi ya 10.
Hata hivyo mwaka 1991 alifanikiwa kumchapa Donovan Ruddock mara mbili.
Tyson ameshinda mapambano 50 akipoteza 6 na mawili alipewa ushindi wa
mezani.