Droo ya kombe la shirikisho Barani Afrika (CHAN) itafanyika tarehe 5 
mwezi ujao kwenye makao makuu ya shirikisho la mpira Afrika yaliyoko 
jijini Cairo nchini Misri.
Jumla ya timu 42 zitapangwa kwenye makundi kulingana na kanda zinapotoka na kila kundi litakuwa linatoa timu tatu.
Timu hizo zitacheza raundi mbili isipokuwa nchi za Libya, morocco pamoja
 na Tunisia ambazo zitacheza zenyewe na kutoa timu mbili zitakazoshiriki
 fainali hizo.
Kanda ya A Magharibi itakuwa na timu za Gambia, Guinea, Guinea Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Senegal and Sierra Leone
Kanda ya Magharibi B itakuwa na makundi mawili ambapo kundi la kwanza 
litakuwa na timu za Burkina Faso, Côte d’Ivoire, Ghana, Niger, Nigeria 
and Togo huku kundi la pili likiwa na  timu za Cameroon, Central African
 Republic, Congo, Chad, DR Congo and Gabon
Kanda ya mashariki itakuwa na timu ya Rwanda ambaye ni mwenyeji, 
Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Tanzania and Uganda lakini 
timu ya Rwanda aihitaji kufuzu maana wao wana nafasi ya uwenyeji.
Kanda ya kusini itakuwa na timu za Angola, Botswana, Comoros, Mauritius,
 Lesotho, Mozambique, Namibia, Seychelles, South Africa, Swaziland, 
Zambia and Zimbabwe
Mechi za kufuzu zitaanza mwezi wa sita hadi mwezi wa nane mwaka huu 
ambapo  timu 15 zitaungana na mwenyeji Rwanda kushiriki michuano hiyo 
ambayo itafanyika mwezi wa kwanza mwaka ujao.
Kwasasa timu ambayo imeshikiria ubingwa huo ni timu ya taifa ya Libya.
