MWANAUMWE NCHINI PAKISTAN AKUTWA NA MKASI WA INCHI 8 TUMBONI MWAKE

Haya ni maajabu mengine…Huyu amekaa na mkasi wa inchi 8 tumboni kwa zaidi ya miaka 12

mkasiiii
Mwanaume mmoja nchini Pakistan amejikuta akiishi na mkasi kwa miaka 12 baada ya kufanyiwa upasuaji na daktari wake na kusahaulika tumboni>>>>
.
Baada ya kuugua tumbo kwa muda mrefu na kukosa hamu ya kula mwanaume  huyo mwenye miaka 53 Karp Ponomarvon aligundua ni kitu gani kilikua kinamsumbua alipofanyiwa uchunguzi.
Kwa maelezo yake alisema tatizo lake lilianza mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo akiwa na tatizo linalofanana na hilo lakini alidharau na kuendelea na maisha kama kawaida na hakuhisi kama ana tatizo lingine lililopelekea kupoteza hamu ya kula na kupoteza uzito kwa haraka hadi alipokwenda hospitali.
Mwezi uliopita aliamua kwenda hospitali na baada ya kufanyiwa upasuaji daktari aligundulika kuna mkasi mkubwa wenye ukubwa wa inchi 8 na daktari aliyekua akimtibu alishangaa kwani alikiri hajawahi kukutana na kitu kama hicho tangu aanze kazi ya kutibu wagonjwa.
Kwa mujibu wa mwanaume huyo alisema haoni sababu ya kuichukulia hatua hospitali iliyohusika kumfanyia upasuaji kwa mara ya kwanza kwani tayari daktari aliyemfanyia upasuaji alistaafu miaka mitatu iliyopita na kwa sasa amefariki dunia na kikubwa anachotaka ni kuona mkasi huo umetolewa na yeye kuwa katika hali nzuri.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

أحدث أقدم

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart