Alichokisema mke wa mchekeshaji Bill Cosby kuhusu tuhuma zinazomkabili mume wake
Habari ambazo zimetawala katika vyombo vya Habari takribani miezi miwili sasa kuhusu mchekeshaji maarufu Duniani>>>>
 Bill Cosby, baada wanawake kadhaa kujitokeza wakidai kuwa Cosby aliwadhalilisha kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma.
Cosby hakuwahi kuzungumza chochote tangu
 madai hayo yaanze kuvuma, jana amezungumza kwa mara ya kwanza vyombo 
vya Habari kuzingatia usawa wakiwa wanaripoti kuhusu taarifa hiyo huku 
akimpongeza mke wake kwa kuwa karibu naye wakati wote tangu kuanza kwa 
matatizo hayo.
Mke wa Cosby, Camille amemtetea mume wake kwa kusema kuwa taswira ambayo imejengwa na vyombo vya habari kuhusu mume wake hajawahi kuiona kwa kipindi chote cha miaka zaidi ya 50 ambayo wamekuwa pamoja.

Camille amesema anampenda na ataendelea kumpenda Cosby licha ya taswira mbaya ambayo amejengewa mume wake huyo.
Bill Cosby anakabiliwa 
na shutuma za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na amekana 
kuhusika na vitendo hivyo na hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la 
kihalifu.