Makundi ya upinzani
nchini Syria yanatarajiwa kukutana nchini Saudi Arabia katika jitihadi
za kuunganisha makundi hayo yanayopigania kumuondoa madarakani rais
Bashar al Assad.
Mkutano huo ambao utafanyika mjini Riyadh una
lengo la kubuniwa kwa kundi ambalo litajadiliana na serikali kuamua
ikiwa mazungumzo ya amani yataendelea.Makundi yaliyoalikwa ni pamoja na kundi la Free Syrian Army linaloungwa mkono na marekani pamoja na makundi mengine ya kiislamu yanayoungwa mkono na Saudi Arabia.
Hata hivyo kundi la wakurdii nchini Syria halijaalikwa na hivyo linafanya mkutano wake.
Vilevile ,Kundi la Islamic State na lile lenye uhusiano na Al Qaeda la Nusra Front pia nayo yametengwa.