Milioni 18 wameathirika na El Nino A.Mashariki

Image copyright AFP
Image caption Wataalam wanasema kwamba watu wasiopungua milioni 18 katika upembe wa Afrika
Wataalam wanasema kwamba watu wasiopungua milioni 18 katika upembe wa Afrika wameathirika na ukame unaotokana na mfumo wa hali ya hewa ya El-Nino...>>>

Mamlaka ya Maendeleola ya Kimataifa IGAD , na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu imeonya kuwepo kwa upungufu mkubwa wa fedha ya kukabiliana na athari za El-Nino.
Watabiri wa hali ya hewa walitabiri athari kubwa kutokana na mvua ya El-Nino kwa miongo kadhaa sasa.Image copyright David Peter via AP Image caption Watabiri wa hali ya hewa walitabiri athari kubwa kutokana na mvua ya El-Nino kwa miongo kadhaa sasa.
Sasa wanasema haijawa mbaya kama waliyokuwa wameogopa.
Lakini mamilioni ya watu katika Afrika Mashariki bado wameachwa katika mazingira magumu.
Takriban watu 100 walifariki dunia kutokana na mafuriko katika maeneo ya kusini mwa Somalia,eneo la kati la Kenya na Uganda .
Vilevile zaidi ya watu nusu milioni wameyakimbia makazi yao.Image copyright Image caption Wale wanaoishi karibu na hari wanakabiliwa na ukame.
Wakati huohuo baadhi ya wakulima walipata mavuno makubwa kutokana na kuimarika kwa viwango vya mvua, ilihali wale wanaoishi karibu na hari wanakabiliwa na ukame.
Nchi zilizoathirika kama Ethiopia zilitumia zaidi ya dola milioni 200 katika jitihada za kutoa misaada lakini mashirika ya misaada yanasema msaada zaidi unahitajika kutoka jumuiya ya kimataifa.
Shirika la Chakula duniani (World Food Programme) linasema wana asilimia 5% tu ya fedha wanazohitaji kusaidia kukabiliana na hali hiyo.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

أحدث أقدم

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart