Arsenal ilikosa fursa ya kuwa sawa kwa pointi na Manchester City katika nafasi ya pili katika ligi ya Uingereza baada ya Swansea kupata ushindi wa dakika za lala salama kufuatia bao lililofungwa ba Bafetimbi Gomez.
Swansea iliihangaisha Arsenal na kufanya mambo kuwa bila bila wakati wa kukamilika kwa kipindi cha kwanza.
Aliyekuwa kipa wa Arsenal Lukasz Fabianski alifanya kazi ya ziada na kuokoa mashambulizi mengi yaliofanywa na Santi Carzola na Aaron Ramsey huku The Gunners wakilivamia lango la Swansea kama nyuki.
Lakini ikiwa imesalia dakika tano Gomis alipiga kichwa kizuri kilichomwacha kipa wa Arsenal bila Jibu huku teknolojia ya mstari wa goli ikisema kuwa David Ospina aliutoa mpira huo baada ya kupita mstari.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger baadaye alisema kuwa ushindi huo wa Swansea haukustahili na kwamba timu yake pia haikuwa na bahati.