Waziri wa fedha awasilisha mwelekeo wa bajeti 2015/2016


                       Waziri wa Fedha SAADA SALUM MKUYA
 
Waziri wa Fedha SAADA SALUM MKUYA amewasilisha mwelekeo wa bajeti kwa mwaka 2015/2016 na kusema kuwa bajeti ya serikali kwa mwaka huu itakuwa ni shilingi TRILIONI ISHIRINI na MBILI ambazo zinatarajiwa kukusanywa na kutumika Katika kipindi hicho.

Akiwasilisha muelekeo wa bajeti kwa wabunge wa jamhuri ya Muungano wa TANZANIA jijini DSM, Waziri MKUYA amesema kuwa Jumla ya Mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa ni zaidi ya shilingi TRILIONI KUMI na NNE ambayo ni sawa na asilimia HAMSINI na SABA nukta NANE ya bajeti yote.

Akiwasilisha mwelekeo wa mapato na matumizi ya serikali ya mwaka 2015/2016 Waziri MKUYA amesema bajeti ya mwaka ujao wa fedha itakuwa zaidi ya shilingi TRILIONI 22.

Kwa upande wake waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu MARY NAGU amewasilisha mpango wa maendeleo ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kwa wabunge waliokutana jijini DSM na kusema mpango huo umezingatia dira ya maendeleo ya taifa.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

أحدث أقدم

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart