Wakrito nchini na watanzania wametakiwa kuliombea taifa.


Wakrito nchini na watanzania wametakiwa kuliombea taifa ili liweze kuvuka salama kipindi hiki kigumu chenye matukio makubwa ya upatikanaji wa katiba mpya pamoja na uchaguzi mkuu huku viongozi wakitakiwa kutenda haki kwani amani ni tunda la haki.
Askofu wa kanisa la AICT dayosisi ya Pwani Charles Salalah ametoa wito huo wakati wa ibada ya ijumaa kuu ambayo kitaifa imefanyika katika kanisa la AICT magomeni jijini Dar es Salaam ambapo amesema maeneo yote duniani ambayo yamekumbwa na machafuko chanzo kikubwa ni ukosefu wa haki hivyo ni wajibu wa kila kiongozi mwenye dhamana kutenda haki.
 
Ibada hiyo imehudhuriwa na wachungaji kutoka madhehebu mbalimbali ambayo pia imetumika kuliombea taifa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo rais Jakaya Kikwete ili mungu amjalie afya njema aweze kuliongoza taifa vyema sala iliyoongozwa na mchungaji Daniel Ntebi.
 
Katika kanisa la KKKT Azania Front ibada ya pasaka imefanyika na kupambwa na maigizo yaliyokuwa yanaonyesha mapito aliyopitia bwana yesu kristo hadi alipokufa msalabani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kifo chake huku waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa ambaye amehudhuria ibada hiyo akizungumzia siku hii.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

Previous Post Next Post

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart