McDonald Mariga Wanyama
|
1987: McDonald Mariga azaliwa
Mariga
Wanyama ni mwanasoka wa aliyeweka rekodi ya kuwa raia wa kwanza kutoka
nchini Kenya kucheza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Rekodi hiyo aliiweka
Machi 16, 2010 akiwa na klabu ya Inter Milan. Alizaliwa jijini Nairobi
akianza soka lake Ulinzi Stars kabla ya kusajiliwa Tusker FC na baadaye
Kenya Pipeline. Sasa anacheza soka nchini Italia akiwa na Parma.
1987: Sami Khedira azaliwa
Sami Khedira
ni mchezaji wa soka kutoka nchini Ujerumani anayeitumikia klabu ya Real
Madrid katika nafasi ya kiungo mkabaji. Alizaliwa mjini Stuttgart.
Mwaka 2010 alitua Los Blancos akitokea VfB Stuggart alikoanzia soka
lake. Hadi sasa anawaniwa na vilabu vya soka vya England kutaka saini
yake mwishoni mwa msimu.
2012: Dubravko Pavličić afariki dunia
Pavličić
alikuwa mlinzi wa kati wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Hércules
(Hispania). Dubravko anakumbukwa nchini Hispania kwani mwaka 1994
aliweka rekodi ya kuifunga Barcelona nyumbani na ugenini wakishinda 3-2
Nou Camp na baadaye 2-1 José Rico Pérez. Alizaliwa Novemba 28, 1967.
Alifariki kwa kansa ya kongosho mjini Elche akiwa na umri wa miaka 44.