Mawaziri
 wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani , Ufaransa , Urusi na Ukrain 
wameelezea wasi wasi uliopo kufuatia kutokea kwa mapigano mashariki mwa 
ukrain na kikiukwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa 
mwezi Februari.
Baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Berlin 
waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier 
aliwaambia waandishi wa habari kuwa kati ya silaha ambazo zitaondoa ni 
pamoja na vifaru.Pande hizo mbili zilionekana kuheshimu makubaliano hayo hadi kulipotokea mapigano ya hivi majuzi kwenye uwanja wa ndege wa Donetsk na kijiji cha Shyrokyne nje ya mji wa Mariupol.
Pande hizo pia zimekubaliana kuendelea kubadilishana wafungwa.
