Mamlaka
ya Nepal inasema kuwa zaidi ya watu 3300 sasa wanasemekana kufariki
katika tetemeko kubwa la ardhi siku ya jumamosi,lakini huku waokoaji
wakiendelea kuyafikia maeneo ya mashambani huenda idadi hiyo
ikaongezeka.
Mamia ya jamii zinazoishi karibu na milima zinadaiwa kuwachwa bila makao lakini harakati za kutaka kuwasaidia zinaendelea.Shrika la umoja wa mataifa linalosimamia watoto UNICEF limesema kuwa karibia watoto millioni moja hawana mahala pa kulala,wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi pamoja na mazingira safi.
Huku athari zaidi za baada ya tetemeko hilo zikionekana,wakaazi wengi waliotishiwa na tetemeko hilo katika mji wa Kathmandu waliamua kulala nje kwa siku ya pili mfululizo ndani ya makaazi ya mda yaliojengwa na mifuko ya plastiki.