Wanafunzi
katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya wanatarajiwa kupelekwa
chuoni humo ili kundoa vitu vyao kabla ya kupelekwa nyumbani.
Serikali ya Kenya imefunga chuo hicho kufuatia shambulio la siku ya alhamisi ambapo watu 150 waliuawa.Uchunguzi kuhusu tukio hilo unandelea na watu wawili zaidi wamekamatwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa wale waliovamia chuo hicho walizungumza lugha ya kiswahili lakini walionekana kupata ushauri kwa njia ya simu za mkononi
Rais wa Marekani Barack Obama amekitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kuahidi msaada wake kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.