Waziri
 wa usalama wa ndani nchini Kenya Generali Joseph Nkaiserry amekiri 
kwamba vyanzo na duru za kijasusi zilitahadharisha lakini zilipuuzwa 
kabla ya shambulizi la Al Shabaab katika chuo kikuu cha Garrissa.
Karibu watu 150 walikufa wakati wa shambulio hilo.Waziri Nkaissery ameongeza kusema shughuli za wokozi zilizofuata pia zilifanywa kiholela.
Baadhi ya Maafisa wakuu wa polisi wamesimamishwa kazi kufuatia shambulia hilo la Chuo Kikuu cha Garrissa.
