Waziri wa Ardi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI
Waziri wa Ardi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI
ameziagiza mamlaka zinazohusika kuwapatia wakaazi wa eneo la kigamboni
jijini DSM hati za kumiliki maeneo yao kuondoa vikwazo na urasimu usio
wa lazima katika kuwapatia wakaazi hao hati hizo.
Waziri LUKUVI ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa wadau wa uendelezaji wa mji mpya wa KIGAMBONI, ambapo amesema mkazi yeyote wa eneo hilo atakayekumbana na vikwazo katika kupata hati hizo awasilishe malalamiko katika ofisi yake ili hatua stahiki zichukuliwe.
Walioudhuria mkutano wa wadau wa uendelezaji wa mji mpya wa KIGAMBONI Jijini DSM, ni baadhi ya wakazi wa mji huo, viongozi wa dini, viongozi wa mkoa wa DSM na Maafisa wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiongozwa wa Waziri wa wizara hiyo WILLIAM LUKUVI.
Waziri LUKUVI akatumia mkutano huu kuelezea masuala kadhaa kuhusiana na uendelezaji wa mji mpya wa KIGAMBONI, hasa ushiriki wa wakazi katika mradi huo. LUKUVI amewashauri wakazi wa KIGAMBONI kuhakikisha hawauzi ardhi zao kiholela na badala yake wanatumia Hati watakazo pewa katika kuingia mikataba yenye tija.
Mradi wa Ujenzi wa Mji mpya wa KIGAMBONI unajumuisha kata Sita ambazo ni KIGAMBONI, TUNGI, MJI MWEMA, VIJIBWENI, KIBADA na Mitaa Miwili ya Kata ya SOMANGILA ambayo ni KIZANI na MBWAMAJI.