Waziri wa uchukuzi SAMUEL SITTA
Waziri wa uchukuzi SAMUEL SITTA amesema serikali inaendelea na
mchakato wa kujenga reli mpya itakayokua na urefu wa kilomita 2,561
itakayoanzia Jijini DSM hadi mkoani KIGOMA kwa kupitia katika miji
kadhaa ambayo itagharibu Shilingi Trilioni kumi na nne, ndani ya miaka
Miaka ijayo.
SITTA ametoa kauli hiyo jijini DSM katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo amesema tayari kampuni ya Usimamizi wa Rasilimali za Reli – RAHCO imekamilisha utaratibu wa kumpata mshauri wa mradi huo.
Waziri SITTA ameongeza kuwa katika mradi huo serikali haitatoa fedha yoyote, ambapo mradi utagharamiwa na benki ambazo zitatoa fedha kama mkopo ambao utarejeshwa kutokana na makubaliano yatakayotokana na tozo ya mizigo itakayopitishwa katika reli hiyo.
Reli hiyo mpya ya kutoka DSM hadi mkoani KIGOMA itapita katika miji ya TABORA, MWANZA, ISAKA hadi RUSUMO, KAILUA – MPANDA – KAREMA na UVINZA hadi MUSINGATI nchini BURUNDI.