Makamu wa Rais Dkt. MOHAMED GHARIB BILAL
Makamu wa Rais Dkt. MOHAMED GHARIB BILAL amesema serikali
itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kujenga na kuboresha
makazi ya watu.
Akizungumza mjini DSM wakati wa uzinduzi wa mpango wa mikopo isiyo na riba ya ujenzi wa nyumba Dkt. BILAL amesema serikali inatambua mchango wa sekta binafsi katika ujenzi wa makazi ya watu kwani bila mchango huo serikali haiwezi kufikia azma ya kujenga makazi bora kwa wananchi.
Dkt. BILAL ametaka ujenzi wa makazi ufanyike katika maeneo yenye miundombinu ya kijamii ikiwemo huduma za maji, barabara, umeme na nyinginezo huku akiwataka wananchi wafuate sheria za mipango miji ili kuepuka kuzagaa kwa makazi yaliyojengwa kiholela.
Mpango huo unatekelezwa na benki ya AMANA kwakushirikiana na kampuni ya property international
Mpango wa mikopo isiyo na riba ya ujenzi wa nyumba unatekelezwa KIGAMBONI, KIBAHA, MLANDIZI na MAFIA ambapo baadaye utatekelezwa ZANZIBAR.