Sebastian Vettel,dereva wa timu ya Ferrari
Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes
Dereva wa mbio za magari wa
timu ya Ferrari Sebastian Vettel amembwaga Lewis Hamilton wa timu ya
Mercedes na kufanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza akiwa na timu hiyo
katika mashindano ya Malaysian Grand Prix. Vettel ameshinda katika
shindano ambalo lilikuwa kali na la kusisimua baada ya Hamilton
kuharibikiwa na tairi kutokana na joto lililotokana na hali ya hewa ya
kitropic na kufanya dereva huyo kushika nafasi ya pili huku nafasi ya
tatu ikienda kwa Nico Rosberg. Ushindi wa mjerumani huyo umemfanya kuwa
ndiye dereva mwenye mafanikio makubwa katika eneo la Sepang akiwa na
mataji manne huku akiwa ni wa 34 wa tofauti katika timu ya Ferrari.