Rais wa zamani wa Misri kuhukumiwa leo

Rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi akiwa gerezani
Rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi akiwa gerezani
Mahakama ya Jinai mjini Cairo Misri, leo inatarajiwa kuendelea kusikiliza kesi ya rais wa zamani Muhammad Morsi ambaye alichaguliwa na wananchi na kupinduliwa na jeshi la nchi hiyo.
Televisheni ya Press TV imeinukuu mahakama hiyo ikitangaza jana kuwa tarehe ya kusikilizwa kesi ya Muhammad Morsi na wanachama wengine 10 wa Ikhwanul Muslimin imesogezwa mbele hadi leo, Machi 26.
Muhammad Morsi na wanachama 10 wa Ikhwanul Muslimin wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo za ujasusi na kulipatia nyaraka za siri shirika la kijasusi la Qatar na televisheni ya al Jazeera ya Qatar.
Nyaraka hizo za siri za Misri ambazo inadaiwa Morsi aliipatia Qatar ni pamoja na taarifa za siri kuhusu jeshi la Misri na taarifa za siri kuhusu siasa za ndani na za kimataifa za Misri.
Kuna uwezekano watuhumiwa hao wakahukumiwa adhabu ya kifo kama watapatikana na hatia.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

Previous Post Next Post

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart