Lionel Messi na Jose Mourinho waongoza kwa utajiri, angalia listi nzima wachezaji na makocha

Lionel Messi ndiye anayeongoza kwenye orodha ya wachezaji matajiri akiingiza pauni milioni 47.8 mwaka 2014
Lionel Messi ndiye anayeongoza kwenye orodha ya wachezaji matajiri akiingiza pauni milioni 47.8 mwaka 2014
Lionel Messi ni mchezaji mpira anayelipwa zaidi kwenye sayari hii, akiingiza karibu pauni milioni moja kwa wiki mwaka uliopita kutokana na posho na mikataba ya udhamini.
Nyota huyo wa Argentina na Barcelona alijiingizia karibu pauni milioni 47.8 mwaka 2014, pamoja na mshahara wa klabu pauni milioni 26 akiongeza pamoja na mikataba ya adidas, FIFA 15 na Ndege za Uturuki.
Kiasi hicho ni pamoja na mshahara wake pamoja na mikataba yake
Kiasi hicho ni pamoja na mshahara wake pamoja na mikataba yake
Inamfanya awe mbele ya nyota wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo ambaye alipata pauni 39.7 milioni mwaka 2014, kwa mujibu wa gazeti la orodha ya wacheza soka tajiri la Ufaransa.
Ronaldo anashika nafasi ya pili akiingiza pauni milioni 39.7
Ronaldo anashika nafasi ya pili akiingiza pauni milioni 39.7
Mchezaji mwezie Messi wa Barcelona Neymar anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pauni milioni 26.8.
Robin van Persie ndiye anayeongoza katika Ligi Kuu ya Uingereza
Robin van Persie ndiye anayeongoza katika Ligi Kuu ya Uingereza
Naye mshmabuliaji wa Man United Robin van Persie ndiye mchezaji aliyeingiza zaidi Ligi Kuu, alikuwa pauni  milioni 18.8 mwaka 2014. Hii ni pamoja na mshahara wa pauni milioni 11.8 pamoja na marupuruou ya pauni milioni 5 yanayotokana na mikataba mbalimbali.
Gareth Bale ambaye ni mchezaji aghali duniani lakini anashika nafasi ya sita
Gareth Bale ambaye ni mchezaji aghali duniani lakini anashika nafasi ya sita
WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI
  1. Lionel Messi £47.8m
  2. Cristiano Ronaldo £39.7m
  3. Neymar £26.8m
  4. Thiago Silva £20.2m
  5. Robin van Persie £18.8m
  6. Gareth Bale £17.5m
  7. Wayne Rooney £16.5m
  8. Zlatan Ibrahimovic £15.8m
  9. Sergio Aguero £15.6m
  10. Robert Lewandowski £14.8m
Jose Mourinho ndiye anayeongoza kwa upande wa makocha aliingiza pauni milioni 31.2 mwaka 2014
Jose Mourinho ndiye anayeongoza kwa upande wa makocha aliingiza pauni milioni 13.2 mwaka 2014
MAKOCHA WANAOLIPWA ZAIDI
  1. Jose Mourinho £13.2m
  2. Carlo Ancelotti £11.4m
  3. Pep Guardiola £11.2m
  4. Arsene Wenger £8.3m
  5. Louis van Gaal £7.3m
  6. Fabio Capello £6.6m
  7. Andre Villas-Boas £6.2m
  8. Sven-Goran Eriksson £5.9m
  9. Jurgen Klopp £5.3m
  10. David Moyes and Laurent Blanc £5.1m
Chanzo: France Football Rich List

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

أحدث أقدم

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart