Nairobi inaongoza miji 20 kama mahali kwenye matumizi makubwa katika masuala ya burudani (starehe).
Taarifa hizo zimethibitishwa katika utafiti wa miji mikuu barani uliofanywa na PricewaterhouseCoopers.
Kuongezeka huko kulihesabiwa kutokana na matumizi ya Sh bilioni 28 mwaka 2013 ambayo yameendelea kuongezeka kwa asilimia 12.5.
Nairobi pia inatajwa kuwa juu kama kitovu cha wawekezaji wa kigeni Afrika, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatano.
Miji mingine ambayo inaongoza kwenye sekta nyingine ni Cairo inaongoza
kwa miundombinu, Tunis, Tunisia mji bora wa watu, wakati Casablanca
inaongoza kwa uchumi.