Mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City watamuuza Yaya Toure msimu
huu katika mpango unaolenga kuwauza wachezaji wengine wa kilabu hiyo
kwa lengo la kununua wachezaji chipukizi watakaoongozwa na mchezaji
Kevin De Bruyn wa Wolfsburg.
Kushindwa kwa kilabu hiyo na Barcelona katika mechi ya kufuzu kwa robo
fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya kumethibitisha kwamba mabadiliko
makubwa yanahitajika katika kilabu hiyo.
Katika wachezaji kumi na moja walioanzishwa katika mechi dhidi ya
Barcelona ni Sergio Aguerro mwenye umri wa maka 26 aliye chini ya umri
wa miaka 27.
Huku Aguerro,Joe Hart,Vincet Kompany,Fernandinho na David Silva wakiwa
na maisha marefu katika kilabu hiyo ,waliosalia huenda wakauzwa.
Hii inamaanisha kwamba Yaya Toure,Bacary Sagna,Martin
Demichelis,Alkesandar Kolarov ,Samir Nasri na James Milner ambaye
kandarasi yake inaisha hatma yao haijulikani.
Kati ya wachezaji ambao hawakuanzishwa katika uwanja wa Nou Camp siku ya
jumatano usiku,Gale Clichy,Pablo Zabaleta,Jesus
Navas,Fernandinho,Steven Jovetic na Edin Dzeko huenda pia wakauzwa.
Frank lampard amesema kuwa anaondoka ili kujiunga na kilabu ya New York City nchini Marekani.