Saud Arabia imeanza operesheni zake za kijeshi nchini Yemen, ikiwa ni kujibu ombi la Rais wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansour Hadi.
Balozi
wa Saudi Arabia Nchini Marekani amesema kuwa, taifa lake na washirika
wao wa ghuba wanatumia mashambulizi ya angani katika harakati za kuunga
mkono serikali halali ya Yemen, ili isichukuliwe na kundi wa waasi la
Houthi.Awali duru zasema kuwa wapiganaji wa Houthi walikuwa wakikaribia kuutwa mji wa Aden, ulioko kusini mwa Nchi hiyo.