Mapigano
makali yameendelea mashariki mwa Ukraine kufuatia majeshi ya serikali
kukabiliana na kundi la Waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na Urusi.
Raia
wanane na wanajeshi wanne wameuawa kufuatia mashambulizi ya silaha kati
ya majeshi ya serikali na Waasi katika mji wa Kramatorsk unaoshikiliwa
na serikali.Hata hivyo mapigano hayo yanakuja huku kukiwa na mpango wa mazungumzo ya amani ili kusitisha mapigano hayo. Vyombo vya habari nchini Urusi vinasema makubaliano ya muda ya kusimamisha mapigano yamefikiwa, japo kuwa hakuna uthibitisho wa serikali. Mapambano bado yanaendelea katika mji wa Debaltseve na wanajeshi wa serikali wa Ukraine wamefanya mashambulizi dhidi ya waasi mashariki mwa Mariupol.