Kiungo
wa kati wa Tottenham Nabil Bentaleb atashiriki katika mechi dhidi ya
Arsenal baada ya kurudi kutoka michuano ya mataifa ya Afrika nchini
Equitorial Guinea....>>>>
Hii inamaanisha kwamba kocha mkuu Mauricio Pochettino ana wachezaji wengi wa kuchagua.
Arsenal itamkosa mfungaji wake wa mabao mengi Alexis Sanchez kutokana na Jeraha la mguu,lakini Danny Welbeck amepona jeraha la paja.
Mechi hiyo imekuja mapema sana kwa kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere huku Alex Oxlade Chamberlain pia akikosekana.