Wapiganaji wa kundi la Alshabaab kutoka Somalia wanasema kuwa wamewaua
watu wanne wanaodaiwa kuwa wapelelezi wa Marekani,Ethiopia na serikali
ya Somalia.
Wanne hao wanadaiwa kupigwa risasi katika mji wa
Baradhere siku ya jumanne baada ya jaji mmoja wa Alshabaab kuwapata na
hatia ya kuwaunga mkono wapelelezi wa CIA na mashirika yanayokabiliana
na kundi hilo.Wiki iliopita maafisa wa Somali wanasema kuwa shambulizi moja la ndege lililotekelezwa na Marekani lilimuua kiongozi wa ujasusi wa Alshabaab Abdishakur Tahlil.