Vikosi vya Libya vyatibua shambulizi>>>
Shambulizi lililolenga kituo muhimu cha mafuta mashariki mwa Libya
halikufua dafu kutokana na mashambulizi ya angani yaliotekelezwa na
vikosi vya serikali vinavyotambuliwa kimataifa.
Kamanda mmoja wa
jeshi la wanahewa anasema kuwa mashambulizi ya angani yaliwalenga watu
wenye silaha waliokuwa wakisonga mbele katika kituo cha mafuta cha
Al-Sidra ambapo watu wengi waliuawa.Zaidi ya miaka mitatu tangu kuanguka kwa utawala wa kanali Muamar Gadaffi serikali hasimu bado zinapigania madaraka nchini Libya.