Hivi ni kweli Beyonce, Jay Z wameiba wimbo wao wa ‘Drunk in Love’? Stori iko hapa
Mwanamke mmoja nchini Hungary amewalalamikia mastaa Beyonce na mumewe Jay Z akidai wamemwibia wimbo wake wa ‘Drunk in Luv‘ ambao tayari aliurekodi na kwa sasa umeonekana kama wa kwao.>>>>
Mwanamuziki Monica Miczura maarufu kama Mitsou alisema Bey na Jay Z pamoja na Producer wao Timbaland waliuchukua mashairi ya wimbo huo aliourekodi mwaka 1995 kisha kuutumia bila ruhusa yake.
Mwimbaji huo alisema ana nithibitisho vyote na anataka alipwe na pia amemtaka mwanasheria wake kuzuia wimbo huo kuendelea kuchezwa mpaka hapo mashtaka yake yatakaposikilizwa.