Taliban yafanya Shambulio kwenye shule Pakistan, waathirika wakubwa ni watoto
Takriban
watu 126, wameuwawa wengi wao wakiwa ni watoto na wengine kujeruhiwa
baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia Shule moja inayomilikiwa na Jeshi
Kaskazini Magharibi mwa Pakistan>>>>
.
Wakuu katika jimbo la Peshawar wamesema
kwamba wapiganaji wapatao sita wenye silaha waliingia katika Shule hiyo
yenye na Wanafunzi 500.
Maafisa usalama wa Pakistan kwa sasa
wamezingira jumba hilo huku milio ya risasi ikisikika, huku jitihada za
kuwaokoa wanafunzi hao zikiendelea.
Waziri mku wa Pakistan amesema watu
zaidi ya 80 wamejeruhiwa wengi wao wakiwa ni watoto chini ya miaka 12 na
16, huku kwa upande wa wapiganaji wawili wa Talebanwakiuawa ikiwemo
mmoja aliyejiua mwenyewe ambapo shambulio hilo likisemekana kuwa ni la
kulipiza kisasi cha Wataleban waliouawa na Vikosi vya Usalama vya Jeshi
la Pakistan.