Taliban yafanya Shambulio kwenye shule Pakistan, waathirika wakubwa ni watoto
Takriban
 watu 126,  wameuwawa wengi wao wakiwa ni watoto na wengine kujeruhiwa 
baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia Shule moja inayomilikiwa na Jeshi
 Kaskazini Magharibi mwa Pakistan>>>>
.
Wakuu katika jimbo la Peshawar wamesema 
kwamba wapiganaji wapatao sita wenye silaha waliingia katika Shule hiyo 
yenye na Wanafunzi 500.
Maafisa usalama wa Pakistan kwa sasa 
wamezingira jumba hilo huku milio ya risasi ikisikika, huku jitihada za 
kuwaokoa wanafunzi hao zikiendelea.
Waziri mku wa Pakistan amesema watu 
zaidi ya 80 wamejeruhiwa wengi wao wakiwa ni watoto chini ya miaka 12 na
 16, huku kwa upande wa wapiganaji wawili wa Talebanwakiuawa ikiwemo 
mmoja aliyejiua mwenyewe ambapo shambulio hilo likisemekana kuwa ni la 
kulipiza kisasi cha Wataleban waliouawa na Vikosi vya Usalama vya Jeshi 
la Pakistan.
