Kama ulipitwa na taarifa ya kauli ya Serikali kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaweza kuisikiliza hapa…
Kufuatia dosari nyingi zilizojitokeza
katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika maeneo mengi nchini Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Hawa Ghasia amesema wote waliohusika kuvuruga uchaguzi huo kwa watawajibishwa hata kama ikiwa ni yeye au ofisi yake.>>>>
“Tumesema
tutafanya uchunguzi na ikibainika kwamba kuna mtu amekosea kwa nafasi
yake kule kwenye Halmashauri tutawachukulia hatua, je ikibainika ni mimi
ambae nimevuruga niko tayari kuwajibika, kama itabainika kuna
Halmashauri haikufanya vizuri kwa sababu mimi ndio nimewafanya wasifanye
vizuri nitawajibika, lakini kama ni wao wenyewe tumewapa maelekezo yote
ya kufanya na wao wamevuruga wao tutawawajibisha…” — Waziri Hawa Ghasia.
Wakati huo huo amesema kuwa katika miaka ijayo uchaguzi huo utakuwa chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, huku akiongeza kuwa uchaguzi huo kugubikwa na kasoro mbalimbali