Hekaheka ya leo December 16 unaweza kuisikiliza hapa, inahusu msichana aliyetupa mtoto chooni
Hekaheka ya leo December 16 inatoka Dar es Salaam ambapo msichana mmoja alijifungua mtoto chumbani kwake ndani ya nyumba aliyopanga na kwenda kumtupa mtoto ndani ya shimo la choo huku akieleza kuwa sababu iliyomfanya aamue hivyo ni kitendo cha mwanaume aliyempa ujauzito huo kumtelekeza.>>>
Mtoto wa mwenye nyumba ambapo msichana
huyo anaishi aligundua kutupwa kwa mtoto huyo baada ya kuingia
kujisaidia katika choo hicho na kusikia sauti ya mtoto akilia kutoka
ndani ya shimo la choo hicho, akamwambia mama yake ambaye alitoa taarifa
kwa mume wake pamoja na mjumbe ambaye alitoa taarifa kituo cha Polisi.
Baada ya Mjumbe kufika na Polisi alikuta
tayari majirani walikuwa wameanza jitihada za kuchimba shimo ili kumtoa
mtoto huyo, baada ya kufanikiwa kumtoa akiwa mzima walimpeleka
Hospitali ya Mwananyamala.
Mtoto huyo ni mzima, baada ya msichana huyo kufikishwa Hospitalini hapo alipewa mtoto wake na kuanza kumnyonyesha.