Hivi ndivyo familia ya Obama ilivyokaribisha msimu wa sikukuu ya Christmas ndani ya White House
Wakati kilele cha sikukuu ya Krismas kikikaribia>>>>
Rais wa Marekani Obama na familia yake walikua wakisherekea pamoja katika uzinduzi wa tamasha la krismas lijulikanalo kama Christmas in Washington Concert ambalo hufanyika kila mwaka.
Obama akiongozana na mkewe pamoja na watoto wake wawili Malia pamoja na Sasha waliweza kusherekea tamasha hilo sambamba na watoto wengine pamoja na watu maalum walioalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika moja ya nyumba za makumbusho ya Taifa.
Likiwa ni tamasha la 33 kufanyika tangu kuanzishwa litapambwa na wanamuzuki mashuhuri pamoja na watoa mada ambao watakua wakizungumzia mambo mbalimbali yanayohusiana na sikukuu ya Krismas.
Lengo la tamasha hilo pia lililenga kusaidia mfumo wa Taifa wa huduma za afya kwa watoto.