Kufuatia
vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa
kupitishwa kwa mswada wa usalama ,mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza
na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo.
Mbunge
huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba
wabunge wengi walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge
mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua nguo.Hivi ndivyo ujumbe huo ulivyosoma katika mtandao wake wa facebook:
''Tulijaribu kulemaza kikao hicho asubuhi yote.lakini ilipofika mwendo wa saa nane waliwasili wakiwa wamejitayarisha ya kutosha.Wabunge wengi walipigwa.Mimi mwenyewe nilipigwa ngumi machoni na mbunge mmoja huku wengine wawili wakijaribu kunivua nguo.lakini mimi si wa kulia lia kwamba nimepigwa kofi! Mbunge aliyenipiga amejua kwamba mimi ni mbunge wa Mbita aliyechaguliwa na wala si kuteuliwa.Walipojaribu kunivua nguo mimi mwenyewe niliwamalizia kuwavulia nguo.Mimi siogopi na nashkuru nilivyoumbwa.Sitakubali kutishwa kwa kutumia jinsia yangu'',aliandika bi Millie..
Maandishi haya baadaye yalifuatiwa na mengine yaliosema kuwa ameenda kupigwa picha na kuangaliwa jicho