Nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo anaweza kukumbwa na
adhabu kutokana na ushangiliaji wake aliouonesha siku ya jumapili
alipofunga goli dhidi ya mahasimu wao wa jadi Barcelona.
Siyo mara ya kwanza Ronaldo kufunga goli kwenye uwanja wa Nou Camp
lakini siku ya jumapili baada ya kufunga alionesha kitendo ambacho
mashabiki wa Barcelona wamedai kuwa alikuwa alikuwa anawatukana.
Mashabiki wamesema siyo mara ya kwanza kwa nahodha huyo wa Ureno
kuonesha kitendo hicho bali imekuwa kawaida yake ya kuwatukana mashabiki
wa upande wa upinzani wakati anapofunga goli, kitendo kama hicho
kilitokea kwenye mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa ulaya msimu
uliopita dhidi ya Atletico mchezaji huyo alivua shati na kuwarushia
mashabiki wa upande wa pili.
Rais wa ligi ya Hispania amesema huwa wanakuwa makini kufatilia ishara
ambazo uoneshwa na wachezaji wanapofunga magoli au pindi mchezo
unapokuwa unaendelea kwahiyo bado wanafatilia na kama itagundulika kuwa
alifanya kosa hilo basi mchezaji huyo atawajibishwa