Michel Platini alichaguliwa tena bila kupingwa kwa muhula wa tatu kaka
rais wa UEFA kwenye kongresi ya mwaka Jumanne, na kudai chombo hicho
kinachotawala soka Ulaya ni bora.
Sepp Blatter aliwekwa kitimoto kama mgeni na alipaswa kuvumilia
kukosolewa kutoka kwa wapinzani wake wanaowania nafasi ya urais FIFA
ambao walitakuwa kufanya uwasilishi wao kwa wajumbe.
Kwa njia nyingi, siku hiyo ilionyesha tofauti katika bodi hiyo inayoongoza soka Ulaya na ile ya dunia.
Wakati UEFA ikipata mafanikio ya kifedha ya Ligi ya Mabingwa, FIFA
imekuwa ikikumbwa na mlolongo wa skandali za rushwa miaka michache
iliyopita.
“Sisi ni wawazi, tuna demokrasia na bora,” Platini aliwaambia waandishi maripota.
UEFA imesema haitomuunga mkono Blatter atakapowania muhula wa tano May
29, ambapo anakabaliwa na upinzani kutoka kwa Luis Figo, Michael van
Praag na Prince Ali Bin Ali Hussein.