Bunge la Afrika kusini liligeuka kuwa uwanja wa vita ambapo wabunge wa
upinzani ilifikia hatua ya kuvutana mashati na maafisa wa usalama na
kufanya wabunge wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF)
wakiongozwa na Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu
na baadae wabunge wengine wa upanzani nao wakatoka nje ya ukumbi.
Sakata
hilo lilizuka wakati Rais wa nchi hio Jacob Zuma alipokuwa akilihutubia
taifa na kuulizwa maswali na wabunge wa chama cha EFF kinachoongozwa na
Julius Malema wakitaka kujua ni lini atarejesha pesa zilizojengea jumba
lake la kifahari la Nkandla.