Misri yaamua kuwaondosha raia wake Libya

wapiganaji wa makundi tofauti nchini Libya
Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ametoa ombi la kuwaondosha kwa ndege raia wa Misri wanaoshi nchini....>>>>
Libya,baada ya wapiganaji wa Jihad kuchapisha picha katika mtandao wakisema wamewateka raia 21 wa kanisa la Coptic.
Picha hizo zinaonyesha watu hao wakiwa wamevalia nguo za rangi ya machungwa wakitembezwa katika ufuo wa bahari na watekaji wao walioficha nyuso zao.
Mtandao huo unaoshirikishwa na kundi la Islamic State umewaelezea watu hao kama wana kampeni wa kanisa hilo la Coptic na kusema kuwa kukamatwa kwao ni kulipiza kisasi kile wanachokitaja kuwa utekaji na unyanyasaji wa wanawake waislamu unaotekelezwa na kanisa la Coptic nchini Misri
Waziri wa ,maswala ya kigeni nchini Misri amewataka raia wa Msri kutosafri nchini Libya.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

Previous Post Next Post

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart