Wapiganaji wa kundi la Alshabaab wamedai kuwaua wapelelezi wanne wa Marekani nchini Somali...>>>>
                    
                
Wiki iliopita maafisa wa Somali wanasema kuwa shambulizi moja la ndege lililotekelezwa na Marekani lilimuua kiongozi wa ujasusi wa Alshabaab Abdishakur Tahlil.
    
 Wapiganaji wa kundi la Alshabaab kutoka Somalia wanasema kuwa wamewaua 
watu wanne wanaodaiwa kuwa wapelelezi wa Marekani,Ethiopia na serikali 
ya Somalia.
Wanne hao wanadaiwa kupigwa risasi katika mji wa 
Baradhere siku ya jumanne baada ya jaji mmoja wa Alshabaab kuwapata na 
hatia ya kuwaunga mkono wapelelezi wa CIA na mashirika yanayokabiliana 
na kundi hilo.Wiki iliopita maafisa wa Somali wanasema kuwa shambulizi moja la ndege lililotekelezwa na Marekani lilimuua kiongozi wa ujasusi wa Alshabaab Abdishakur Tahlil.
